TWENDE BUTIAMA 2024

Tarehe 29 Septemba, 2024 msafara wa Twende Butiama kwa mwaka huu ulianza rasmi jijini Dar es salaam kuelekea Mwitongo Butiama, msafara huu umetumia siku 15 na kutembea mikoa12, kupanda miti zaidi ya 5,000 na kutoa misaada ya madawati na vifaa tiba katika maeneo msafara huo ulipopita.

ABC Bicycle moja kati ya wadau waliounga mkono msafara huu kwa mwaka huu, tumewezesha msafara huu kwa kutimiza lengo lake la kufika Butiama kwa kutoa ufundi katika siku zote za msafara huo na kutoa ushauri wa utumiaji mzuri wa Baiskeli katika msafara huo.

Kwa mwaka huu 2024 katika kuwezesha msafara huo tulikuwa na kliniki ya ufundi wa Baiskeli ambayo ilifanyika kwa wiki nzima kuanzia tarehe 23 septemba hadi 28 septemba kwa waendesha Baiskeli wote wa msafara huo kujiandaa kwaajili ya kuweka baiskeli zao sawa ili kuanza msafara huo.

ABC Bicycle tunashukuru watu wote walioshiriki msafara huu kwa mwaka huu na wadau wote waliowezesha kufanikisha kufikia lengo la msafara huu wa Twende Butiama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Shopping Cart0

Cart