TWENDE BUTIAMA, 2022

Twende Butiama ni msafara wa waendesha Baiskeli nchini Tanzania ambao hufanyika kila mwaka, kutoka jiji la Dar es Salaam hadi Butiama kwa Hayati Mwl. Julius K. Nyerere kama namna ya kuenzi yale Mwalimu aliyehusia wakati wa uhai wake.

Mwaka huu wa 2022, msafara ulianza tarehe 02 Oktoba hadi 14 Oktoba ambapo ulihitimishwa pale Butiama.

Kampuni ya ABC Bicycle ilihusika kwa mambo makuu mawili ndani ya msafara huu. Moja ikiwa ni kutoa huduma ya ufundi kwa msafara mzima kuanzia Dar es Salaam hadi Butiama, na pili utoaji wa madawati 10 katika Shule ya Msingi Medeli iliyopo jijini Dodoma kama moja ya wafadhili wa zoezi hili.

Lengo ni kuenzi yale Hayati Mwl. Nyerere aliwahi kuyahusia ikiwa ni pamoja na kumshinda adui Ujinga.

Ungetamani kuona tunashiriki vipi TWENDE BUTIAMA, 2023?

Previous Post
Newer Post

1 Comment

  • israelnightclub.com

    May 15, 2023 - 7:57 pm

    Itís nearly impossible to find educated people in this particular subject, however, you seem like you know what youíre talking about! Thanks

Leave A Comment

No products in the cart.

X