Arusha bicycle center ni kampuni inayohusika nakuuza baiskeli na vipuli vyake toka nchi ya uswiss kwa jumla na rejareja ,Ambayo makao yake makuu ni Olasiti Arusha.Uwongozi wa Arusha bicycle center unapenda kuujulisha umma kuwa

Tunatafuta vijana(wakike/wakiume) sita (6) wanaopenda kujifunza maswala ya ufundi wa baiskeli kutoka maeneo mbalimbali Tanzania.
Mafunzo ya ufundi baiskeli yatachukua muda wa takribani mwaka mmoja, bila malipo ya ada yeyote, wahitimu watakabidhiwa vyeti .
Mwombaji ataambatanisha CV, vyeti na barua ya maombi.

Maombi yatawasilishwa ofisini kwetu au kutumwa katika barua pepe mechanics.abc@gmail.com
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 4/6/2016.
Kwa maelezo zaidi kuhusu ABC tembelea ukurasa wetu wa facebook: Arusha Bicycle Center, Simu: +255764056791,+255767520790

VIGEZO

  1. Awe amehitimu kidato cha nne nakuendelea, kiwango kizuri cha ufaulu kitapewa kipaumbele.
  2. Awe anajua kuendesha baiskeli na mpenda mazoezi.
  3. Awe na uwelewa wa kompyuta, mwenye cheti ufaulu wa kiwango kizuri atapewa kipaumbele.
  4. Awe anapenda ufundi wa baiskeli, mwenye ufahamu wa baiskeli atapewa kipaumbele.
  5. Awe ni mwongeaji wa lugha ya kiingereza, mwongeaji mzuri atapewa kipaumbele.
  6. Awe mwaminifu, msikivu, anajiamini, mdadisi wa mambo na mfanya kazi kwa bidii.
  7. Awe na umri kati ya miaka 18-25.
  8. Wasichana watapewa kipaumbele.
  9. Awe na uwezo wa kujiongoza na kuongoza wengine.
  10. Mwenye elimu ya ujasiriamali atapewa kipaumbele.
Newer Post

No products in the cart.

X