Disemba 21, mwaka 2022 Kampuni ya ABC Bicycle Company Limited ilishiriki kwa kuwashika mkono waendesha Baiskeli wa msafara wa Pedal To Ngorongoro, kama namna ya kutamatisha mwaka.

Msafara wa Pedal to Ngorongoro hufanyika mara 1 kwa mwaka ambapo kwa mwaka 2022 ilikua mara ya pili, ukianzia Dar es Salaam na kumalizika katika Hifadhi ya Taifa, Ngorongoro.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ABC Bicycle Company Limited Ndg. Hans Harrison alimkabidhi bahasha kiongozi wa msafara Ndg. Hillary Temu kwa lengo la kufanikisha safari yao.

Msafara huu uliweka kambi katika eneo la Meserani Snake Park, mkoani Arusha kabla ya kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.

ABC Bicycle Company Limited itaendelea kushirikiana na wadau wote wa Baiskeli, kuhakikisha misafara yote ya Baiskeli inafanikiwa, pia uuzwaji na utengenezaji wa Baiskeli.

Tunawatakia Kheri ya Mwaka Mpya wa 2023.

Previous Post

Leave A Comment

No products in the cart.

X